Kiswahili | English
Site Keyword Search:
    
 
Total site visits: 3711971.DK. BILAL MGENI RASMI SIKU YA MAZINGIRA

MAKAMU WA RAIS DKT. MOHAMMED GHARIB BILAL KUWA MGENI RASMI KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal  Aprili Mosi, 2011 anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika siku ya Mazingira Duniani inayoadhimishwa kitaifa mkoani Ruvuma katika mji wa Songea. Makamu wa Rais Dkt Bilal anamwakilisha Rais Jakaya Kikwete katika maadhimisho hayo ambayo ujumbe wake Kimataifa ni MISITU NI TUNU YA ASILI. Kwa upande wa Tanzania moto ya siku hiyo kwa mwaka huu ni MIAKA 50 YA UHURU, PANDA MITI NA KUITUNZA: HIFADHI MAZINGIRA.

Katika maadhimisho hayo Makamu wa Rais anatarajia kuzungumzia hali ya Mazingira nchini kwa miaka 50 tangu uhuru, Mazingira ikiwa ni moja ya Idara/Wizara iliyochini ya Ofisi yake. Sambamba na shughuli hiyo Makamu wa Rais atapata fursa ya kukagua mabanda mbalimbali katika Uwanja wa Majimaji ambapo pia atapata kusikia salamu maalum za Mkoa wa Ruvuma katika maadhimisho hayo ambayo yataambatana na ujumbe kutoka kwa Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Mazingira Dkt. Terezya Huvisa.


Array
 

<< View list of Announcements.