Kiswahili | English
Site Keyword Search:
    
Total site visits: 3711970.

Benki ya Wananchi Njombe yazinduliwa

Benki ya Wananchi Njombe yaaswa kubuni huduma zitakazowakwamua wananchi katika umaskini. Na Mwandishi Maalum – Iringa Jumatano – Feb 29, 2012  

Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal ametoa changamoto kwa Benki ya Wananchi Njombe kufikiria kuhusu kubuni huduma ambazo zitakuwa nafuu na zinazoweza kuwasaidia wananchi kujikwamua katika umaskini. Akizindua  Benki hiyo jana wakati wa ziara yake ya kikazi wilayani Njombe Dk. Bilal alisema anafahamu wazi kuwa lengo lao la kwanza ni kujenga mtaji na kuwataka lengo hilo lisiwafanye kusahau kuwa jukumu lao la kwanza ni kuwanyanyua wananchi kimtaji. Alisema wananchi wanaowalenga ni maskini na wale wenye uchumi wa kati ambao mahitaji yao siku zote huwa tofauti na wale wenye mali kwa kuwa wanahitaji mikopo ya muda mrefu yenye riba nafuu. “Mkiweza kuwasaidia wananchi hawa kwa kuzingatia maisha na mazingira wanayoishi naamini mtafanikiwa sana na wao watathamini nafasi yenu katika maisha yao,” alisema Dk. Bilal. Aidha, Makamu wa Rais aliwataka watumishi wa Benki hiyo kuhakikisha wanajenga uwazi, ukweli na umakini katika kazi zao na wanakuwa na tabia ya kuwaheshimu na kuwachangamkia wateja ili waweze kubaki na walengwa wao na watoe taarifa zao kwa wanahisa kwa wakati.

Aliwakumbusha pia umuhimu wa kutangaza taarifa hizo kwa wananchi ili waweze kwenda katika Benki hiyo kutumia huduma zao na kusisitiza lengo lao liwe kujitanua katika maeneo ya vijiji ambayo yana wananchi wengi wanaohitaji mchango wa sekta ya benki katika kukuza kazi zao. Mwenyekiti wa Bodi ya Benki hiyo Twilumba Ulaya alimweleza Makamu wa Rais kuwa mwitikio wa wananchi juu ya kuanzishwa kwa Benki ya Wananchi Njombe ni mkubwa kwani hadi kufikia Januari 31, 2012 jumla ya akaunti 5,199 zenye jumla ya amana za shilingi bilioni 1.8 zilikuwa zimekwisha funguliwa.

Aidha alisema katika kipindi hicho jumla ya hisa 442,716 zenye thamani ya shilingi milioni 442.7 zilikuwa zimeuzwa na mikopo ipatayo 2,313 yenye thamani ya shilingi bilioni 3.6 imetolewa kwa wananchi. Twilumba alisema benki hiyo ambayo ilianzishwa Septemba 13, 2010 inakabiliwa na changamoto ya kuwa na mtaji mdogo na hivyo kuiomba serikali ione uwezekano wa halmashauri zote nchini kutumia Benki za Wananchi ili benki hizo ziweze kuimarika kwa haraka kutokana na ushindani. Pia, aliiomba serikali kupitia Benki Kuu kupunguza masharti ya kuanzisha Benki za Wananchi na benki hiyo ipatiwe gari ili waweze kuwafikia wananchi wengi hasa waishio vijijini.

veysel karani hz mehdi recent business newsmagazine newsfirst class business all places haber cook recipe

Array
 
<< View list of Announcements.