Kiswahili | English
Tafuta Tovuti hii kupitia hapa:
    
 
Total site visits: 4012513.                                                      

Maliasili nchini Tanzania ni chanzo kukubwa cha ustawi wa maisha ya wananchi na ni uti wa mgongo wa sekta kuu za uzalishaji kama vile kilimo, utalii, uvuvi na madini. Uhusiano baina ya ukuaji wa uchumi na usimamizi wa mazingira na maliasili umetiliwa mkazo katika Sera ya Taifa ya Mazingira na Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania (MKUKUTA). Aidha, usimamizi endelevu wa mazingira ni mojawapo ya vipengele 8 vilivyoorodheshwa katika Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs). Vile vile, katika hotuba ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipokuwa akizundua Bunge mwezi Desemba 2005, alitaja changamoto za mazingira kuwa ni mojawapo ya maeneo 10 ya vipaumbele vya Serikali ya Awamu ya Nne ambavyo vinatakiwa kutiliwa mkazo. Kufuatilia maazimio haya, mwezi Machi 2006 Serikali ilipitisha Mkakati wa Kuhifadhi Mazingira ya Ardhi na Vyanzo vya Maji ili kusimamisha uharibfu wa mazingira ya ardhi na kutunza vyanzo vya maji nchini.

 

Maamuzi sahihi katika usimamizi wa mazingira yanahitaji takwimu za uhakika na sahihi kuhusu Hali ya Mazingira nchini. Aidha, takwimu hizo zinatakiwa kupatikana kwa wakati muafaka. Ni kutokana na hali hii kwamba Sheria ya Usimamizi wa Mazingira (2004) kifungu cha (1) kinaelekeza kuandaliwa kwa Ripoti ya Hali ya Mazingira nchini kila baada ya miaka miwili ili kusaidia katika utoaji wa maamuzi sahihi kuhusu usimamizi wa mazingira.

Ninahimiza kila mdau kushiriki katika hifadhi ya mazingira ili kuboresha hali ya maisha kwa kuzingatia mazingira endelevu kwa ajili ya vizazi vilivyopo na vizazi vijavyo. Jukumu hili ni la kila mmoja; timiza wajibu wako.

Dkt. Batilda S. Burian
WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS - MAZINGIRA