KATIBU MKUU OFISI YA MAKAMU WA RAIS AZINDUA KAMATI YA URATIBU WA VVU/UKIMWI NA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA MAHALI PA KAZI.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Joseph Malongo hii leo amezindua Kamati ya uratibu VVU/UKIMWI na magonjwa yasiyoambukizwa mahali pa kazi. Uzinduzi huo umefanyika hii leo katika Ofisi ya Makamu wa Rais Mtaa wa Makole, Jijini Dodoma. Kamati hiyo inahusisha wajumbe kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Kitengo cha Anuai za Jamii.

Mhandisi Malongo amewataka wajumbe hao kutoa hamasa kwa watumishi wenzao kufanya mazoezi na kupima afya zao mara kwa mara ili kuepuka magonjwa yanayoweza kuzuilika.