MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AMJULIA HALI WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII ALIYELAZWA MUHIMBILI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amemtembelea Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Hamisi Kingwangalla aliyelazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam ambapo alimjulia hali na kumpa pole kufuatia ajali ya gari aliyoipata Agosti 4, 2018 huko Manyara.