Kiswahili | English
Site Keyword Search:
    
 
Total site visits: 3378129.Listed below are the latest items of news:
KAMPUNI YA THE NETWORK YATOA MILIONI 100 KUSAIDIA SHUGHULI ZA MAZINGIRA

 

Mwakilishi wa Kampuni ya The Network Bw. Sebastian Maganga ikikabidhi mfano wa hundi kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba. Kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Eng. Joseph Malongo

Posted: 17th Nov 17

KATIBU MKUU NA NAIBU KATIBU MKUU WAPOKELEWA OFISI YA MAKAMU WA RAIS

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January akiongea na viongozi wa Menejimenti pamoja na Katibu Mkuu Mhandisi Joseph Malongo na Naibu Katibu Mkuu Bi. Butamo Kasuka mara baada ya kuapishwa Ikulu - Dar es Salaam.

Posted: 28th Oct 17

KATIBU MKUU OFISI YA MAKAMU WA RAIS AKABIDHIWA OFISI RASMI

 

 Katibu Mkuu mpya wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhandisi Joseph K. Malongo(kulia) akipokea hati ya makabidhiano kutoka kwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Prof. Faustin Kamuzora Ofisini mtaa wa Luthuli.

Posted: 31st Oct 17

MHE. KANGI LUGOLA AZINDUA OPERESHENI YA USAFI

 

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Kangi Lugola (Mwenye tracksuit) hii leo ameshiriki katika uzinduzi wa Operesheni maalumu ya kusafisha mazingira kote nchini. Zoezi la uzinduzi limefanyika Tandale kwa Ali Maua jijini Dar es Salaam.

Posted: 30th Oct 17

MHE. MAKAMBA AKUTANA NA VIONGOZI WA TAASISI ZA MUUNGANO

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. January Makamba wa (tano kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Taasisi za Muungano waliopo Zanzibar. Waziri Makamba amepata fursa ya kuwasilikiza na kuwaahidi kufanyia kazi mapendekezo yote yaliyowasilishwa.

Posted: 21st Oct 17

MKUTANOWA 23 WA NCHI WANACHAMA WA MKATABA WA MABADILKO YA TABIANCHI, BONN, UJERUMANI

 

 Mkurugenzi  wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bwana Richard Muyungi (kulia) na Dr.  Fabian Madele (kushoto)   Mwingine ni  Dr. Paul Desanke mratibu wa masuala ya kuhimili mabadiliko ya tabia nchi kwa nchi zinazoendelea  katika Mkutano mjini  Bonn, Ujerumani wakiwa na  Gavana  Arnold Schwarzenegger .

Posted: 15th Nov 17

NAIBU WAZIRI LUGOLA AWASILI OFISI YA MAKAMU WA RAIS

 

Naibu Waziri Mhe. Kangi Lugola  akisalimiana na Mkurugenzi wa Mazingira Bw. Richard Muyungi mara baada ya kuwasili katika Ofisi ya Makamu wa Rais, kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Prof Faustin Kamuzora

Posted: 10th Oct 17

NAIBU WAZIRI MH. KANGI LUGOLA AKILA KIAPO - IKULU

 

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Kangi Lugola akila kiapo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dar es Salaam, kufuatia mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri yaliyofanywa na Mhe. Rais hivi karibuni

Posted: 12th Oct 17

NAIBU WAZIRI MH. KANGI LUGOLA AKUTANA NA WATUMISHI WA OFISI YAKE

 

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Kangi Lugola akizungumza na sehemu ya watumishi wa Ofisi ya Dar es Salaam na kuwaasa kufanya kazi kwa bidii, umoja, na kuhakikisha kila mtu anatimiza wajibu wake. Mkutano huo umefanyika Mtaa wa Luthuli Dar es Salaam.

Posted: 17th Oct 17

OFISI YA MAKAMU WA RAIS YAANDAA WARSHA YA KUJENGA UWEZO KWA TAASISI KATIKA UDHIBITI WA KEMIKALI

 

 Mgeni Rasmi katika warsha hiyo Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bwana Richard Muyungi (waliokaa katikatii akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe waliohudhuria warsha hiyo kutoka Taasisi mbalimbali za Serikali.

Posted: 31st Oct 17

SERIKALI KUENDELEA NA MIRADI YA MABADILIKO YA TABIANCHI

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akikagua eneo lililopandwa miti aina ya mikoko katika eneo la Kisakasaka Unguja. Azma ya Serikalini kuhakikisha maendeleo endelelevu kwa wananchi wake ikiwa ni pamoja na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi. Kulia ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mazingira Bw. Sheha Mjaja

 

Posted: 21st Oct 17

UGENI KUTOKA BENKI YA DUNIA WAMTEMBELEA PROF. KAMUZORA

 

Prof. Faustin Kamuzora (Katikati) Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais mara baada ya kukutana na ugeni kutoka Benki ya Dunia. Watatu kutoka kulia ni Naibu Katibu Mkuu Eng. Ngosi Mwihava. Pamoja na mambo mengine ugeni huo uliwasilisha taarifa yao mara baada ya kutembelea Mradi wa Kihansi hivi karibuni.

Posted: 16th Oct 17

VIONGOZI WA TIMU YA MAJIMAJI WAMPA TUZO WAZIRI MAKAMBA

 

Viongozi wa timu ya Majimaji  wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhi tuzo maalumu kwa Waziri Makamba kwa kutambua mchango wake katika kukuza timu yao na kuwasaidia kupata ufadhili. 

Posted: 17th Nov 17

WAZIRI MAKAMBA AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA SWEDEN

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba (kushoto) akibadilishana mawazo na Balozi wa Sweden Nchini, Katarina Rangnitt (kulia) Katikati ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustin Kamuzora.

Posted: 12th Oct 17

WAZIRI MAKAMBA AKUTANA NA BALOZI WA NORWAY

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba hii leo amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Norway nchini  Tanzania Hanne-Marie Kaarstad (katikati) Mtaa wa Luthuli jijini Dar es Salaam. Pamoja na mambo mengine wamejadili namna ya kuendelea kushirikiana katika sekta ya Hifadhi na Usimamizi endelevu wa mazingira nchini.

Posted: 16th Oct 17

WAZIRI MAKAMBA AKUTANA NA JUMUIYA YA WAFANYABIASHARA ZANZIBAR

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais  Muungano na Mazingira Mhe January Makamba akifafanua jambo mbele ya  kusanyiko la wanajumuiya ya Wafanyabiashara wa Zanzibar. Kikao hicho kimefanyika hii leo eneo la Kinazini Zanzibar. Wengine katika picha ni viongozi wa Jumuiya hiyo.

Posted: 19th Oct 17

WAZIRI MAKAMBA ATEMBELEA BANDARI, TRA NA ZRB ZANZIBAR

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais  Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akiwa katika kikao na Menejimenti ya Bodi ya Mapato Zanzibar. Wa pili kushoto ni Kamishna wa Bodi Bw. Amour Hamil Bakari na Bi. Khadija Shamte  Naibu Kamishna. Waziri Makamba yuko ziarani Zanzibar kutembelea Taasisi za Muungano na zile zisizo za Muungano.

Posted: 19th Oct 17

WAZIRI MAKAMBA AWASILISHA TAARIFA MBELE YA KAMATI YA BUNGE YA KATIBA NA SHERIA

 

Mhe. January Makamba akiwa na viongozi wakuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais mara baada ya kuwasilisha taarifa ya Utekeleji wa Kamati ya pamoja ya SMT na SMZ, kikao kimefanyika Dodoma.

Posted: 2nd Nov 17

  
 

30th Nov -1