Kiswahili | English
Site Keyword Search:
    
 
Total site visits: 3960311.MAWAZIRI SABA WAKUTANA KUJADILI KUTOKOMEZA UVUVI HARAMU

 

 MAWAZIRI SABA WAKUTANA KUJADILI NAMNA YA KUTOKOMEZA UVUVI HARAMU

Mawaziri saba wakiongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba wamekutana Leo jijini Dar as Salaam ikiwa ni agizo la Mhe Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ili kujadili namna ya kudhibiti na kukomeza kabisa uvuvi haramu hususan uvuvi wa kutumia mabomu.

Akifungua mkutano Mwenyekiti Waziri mwenye dhamana ya mazingira Mhe. January Makamba ameeleza kuwa kumekuwa na wimbi kubwa la uvuvi haramu hasa katika maeneo yanayopakana na bahari ya Hindi ambao unaleta uharibifu mkubwa wa mazingira ya Bahari kwa kuharibu matumbawe viumbe hai baharini na kuharibu rasilimali ya utalii.

Mkutano huo umehudhuriwa na Mawaziri kutoka sekta husika ikiwa ni pamoja na Wizara ya uvuvi, Ulinzi, Mambo ya Ndani, Ofisi ya Rais -Tamisemi, Uchukuzi na Wizara ya Maliasili na Utalii.

 


 

<< Back to News Archive.