Kiswahili | English
Site Keyword Search:
    
 
Total site visits: 3776738.WAZIRI MAKAMBA AKUTANA NA KAMATI YA BUNGE YA VIWANDA, BIASHARA NA MAZINGIRA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. January Makamba hii leo amekutana na Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira katika kutoa taarifa za utekelezaji wa maagizo ya Kamati.

Kamati inakutana na wataalamu kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira pamoja na wale wa Ofisi ya Makamu wa Rais, ambapo kwa siku ya kwanza Kamati imepokea taarifa ya Hali ya Mazingira katika Mito na Mabonde na taarifa ya Hali ya Mazingira katika Madampo hapa nchini.

Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Dkt. Diodorus Kamala ameipongeza Serikali kwa jitihada za kukabiliana na changamoto za hifadhi ya mazingira hapa nchini na kuwataka kuongeza bidii na juhudi zaidi katika  suala hilo lenye msukumo mkubwa, kitaifa, kimataifa na kwa ustawi wa wananchi wa sasa na vizazi vijavyo.

 


 

<< Back to News Archive.