Kiswahili | English
Site Keyword Search:
    
 
Total site visits: 3784841.WAZIRI MAKAMBA AKUTANA NA JUMUIYA YA WAFANYABIASHARA ZANZIBAR

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais  Muungano na Mazingira Mhe January Makamba ameanza ziara ya kikazi ya siku saba visiwani Zanzibar. Katika siku ya kwanza Mhe. Makamba amepata fursa ya kukutana na kufanya mazungumzo na Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Zanzibar kwa lengo la kubadilishana uzoefu, kubaini fursa na changamoto zinazowakabili na kuona namna bora ya kupata ufumbuzi.

Miongoni mwa changamoto zilizojadiliwa na kuwekewa mikakati ya utekelezaji ni pamoja na masuala ya kodi, namna ya kunufaika kutoka na fursa zilizopo baina ya pande zote mbili za Muungano na kuondoa vikwazo vinavyotokana na changamoto hizo ili kuleta ufanisi.

Mhe. Makamba amewahakikishia wana juimuiya hao kuwa Ofisi yake itaratibu vikao kati ya Ofisi yake na wafanyabiashara hao ili kupata fursa ya kutoa mrejesho wa utekelezaji wa mambo waliyokubaliana.

Mbali ya kukutana na wafanyabiashara hao Waziri Makamba pia amepata fursa ya kutembelea Vyombo mbalimbali vya Habari hapa Unguja kutoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya Muungano. Vyombo vilivyotembelewa ni pamoja na Zenji FM na Zenji Tv, Bahari FM na Cocunut FM.

Ziara ya Waziri Makamba katika siku pili atatembelea Miradi mikubwa ya Mazingira na kuwa na Vikao na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRB).


 

<< Back to News Archive.