Kiswahili | English
Site Keyword Search:
    
 
Total site visits: 3954735.KAMPUNI YA THE NETWORK YATOA MILIONI 100 KUSAIDIA SHUGHULI ZA MAZINGIRA

Kampuni ya The Network yaipatia Ofisi ya Makamu wa Rais hundi ya Shilingi Mia Moja kwa ajili ya Masuala ya Mazingira


Waziri wa Nchi wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba hii leo amepokea mfano wa hundi yenye thamani ya kiasi cha Shilingi Milioni Mia Moja , pesa zilizotokewa na Kampuni ya The Network kwa ajili ya masuala ya Mazingira nchini.

Mwakilishi wa Kampuni ya The Network Bw. Sebastin Maganga amesema kuwa kampuni yao imeona ni vema kuwekeza katika suala la Mazingira kutokana na kuwa ni suala mtambuka na linagusa maisha ya kila mmoja wetu.
“Sisi The Network tumeamua kujikita katika eneo ambalo ni muhimu zaidi na kuhakikisha yale tuliyoyarithi kwa babu zetu tunayaendeleza na kuhakikisha jamii inafanya shughuli za kimaendeleo za kiuchumi na za kijamii, hivyo ni lazima kuanza katika eneo lenye umuhimu mkubwa kijamiii, Maganga alisisitiza.

Aidha Bw. Maganga amesema kuwa changamoto za kimazingira zitafikiwa ufumbuzi ikiwa wadau kama wote wakahakikisha wanajikita katika kuzipatia ufumbuzi maana sio zoezi la mtu mmoja. Kwakuwa wajibu wa kuifanya Tanzania bora leo, kesho na kesho kutwa si wajibu wa Mheshimiwa Waziri tu ni wajibu wa kila mmnoja wetu, kwa mchango wake mdogo mdogo.

Nae Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Muungano na Mazingira, ameishukuru kampuni ya the network kwa kuuamua kuichangia Ofisi ya Makamu wa Rais katika jitihada za hifadhi ya mazingira, na kusisitiza kuwa ni kampuni ya kwanza inayojishughulisha na michezo ya kubahatisha kuchangia katika eneo hilo na kusema kuwa ni mwanzo mzuri na utaacha kumbukumbu ya kudumu.

Waziri Makamba amesema kuwa pesa hizo zitamumika katika kuifanya Dodoma kuwa mji wa kijani na kupendeza kwa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii (kwa maana ya Wakala wa Misitu), wakala wa mbegu wa taifa, Uongozi wa Mkoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa, wataounda kikundi kazi kwa ajili kuja na mbinu na mikakati ili kuwezesha mji wa Dodoma upendeze.

 

<< Back to News Archive.