Kiswahili | English
Site Keyword Search:
    
 
Total site visits: 3784832.Mkutano wa Mawaziri wa Afrika kuhusu Mazingira

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Mohammed Gharib Bilal akizungumza na Bibi Christiana Figueres, Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia Nchi yenye Makao yake mjini Bonn, Ujerumani. Mazungumzo hayo yalifanyika jijini Arusha wakati Makamu wa Rais alipofungua Mkutano wa Mawaziri wa Afrika kuhusu Mazingira unaoendelea jijini hapo. Katika Mazungumzo hayo, Bibi Figueres alimueleza Mheshimiwa Makamu wa Rais kuwa, Umoja wa Mataifa unatambua mchango wa Tanzania katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya Tabia nchi na kwamba jitihada za Tanzania katika kuhifadhi mazingira ni mfano kwa nchi nyingi Duniani. Kwa upande wake, Mheshimiwa Makamu wa Rais alimueleza Bibi Figueres kuwa, Tanzania inakabiliwa na changamoto kubwa katika kuhifadhi mazingira sasa kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu na hivyo serikali ya Tanzania bado inahitaji ushirikiano wa dhati kwa wadau wa mazingira duniani ili kusaidia nchi ibakie na mazingira sadifu kwa ajili ya vizazi vijavyo.

Imetolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais. 14 sept 2012.


 

<< Back to News Archive.