Kiswahili | English
Site Keyword Search:
    
 
Total site visits: 3960923.UZUIAJI WA UTUPAJI OVYO TAKA ZA HOSPITALI USIO WA KITAALAMU

 JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA MAKAMU WA RAIS

 

 

 

 

TANGAZO KWA UMMA

UZUIAJI WA UTUPAJI OVYO TAKA ZA HOSPITALI USIO WA KITAALAMU

 

Sheria ya usimamizi wa Mazingira ya mwaka 2004 inapiga marufuku uchafuzi wa mazingira ikiwa ni pamoja na taka za hospitali. Aidha Kanuni za Taka Hatarishi za mwaka 2009, zinasisitiza utenganishi wa taka mbalimbali zitokazo kwenye hospitali kwa kuzitibu katika namna ambayo haitaleta athari katika mazingira na afya ya binadamu. Pia Kanuni zinahimiza matumizi ya teknologia sahihi kama vile matumizi ya incinerators ambazo huchoma taka za hospitali na kuziteketeza kabisa.

 

Ofisi yangu imefuatilia na kugundua kuwa taka nyingi za hospitali, taka kutoka katika maduka ya madawa zilizoisha muda wake zinatupwa ovyo  au kuharibiwa kwa utaratibu usiokubalika kitalaamu. Tumefuatalia na kukuta malundo ya madawa chakavu na vifaa vya hospitali vilivyotumika katika maeneo ya visiwa vya Bongoyo na Mbudya. Aidha madawa chakavu yanatupwa holela katikadampo la Pungu Kinyamwezi. Hii ni hatari sana kwa mazingira na kwa afya ya binadamu. 

 

Kuanzia sasa ni marufuku kutupa taka hizi katika utaratibu usio wa kawaida. Kila hospitali na zahanati au kituo cha afya kihahakikishe kinatumia incinerators  au utaratibu mwingine uliosahihi kwamujibu wa sheria ya mazingira na kanuni zake. Aidha ninaiagiza NEMC kuanzia sasa wafanye msakomkali kubaini hospitali na watu wanaokiuka agizo hili. Nimewapa mwezi mmoja na kwa  wale wanaofanya hivyo waache mara moja.   Kwa msako huu atakayebainika kukiuka hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

 

Nichukue fursa hii kutoa tena pole kwa wezentu wa Mkoa wa Kagera na maeneo ya jirani kwa athari za tetemeko la ardhi.

Baada ya tatetemeko kuna athari kubwa zakimazingira ambazo zimejitokeza. Hivyo mimi binafsi ninafuatilia suala hili kwa ukaribu na kuhakikisha athari ambazo zimejotokeza na zinazoendelea kujitokeza zinashughulikiwa kwa haraka.  Nimeagiza Ofisi yangu pamoja na NEMC washirikiane kwa ukaribu sana na watendaji wa Mkoa na Kamati mbalimbali zilizoundwa kushughulikia maafa haya na kufanya tathmini ya athari za mazingira zilizojitokeza na kuelekeza hatua za haraka kuchukuliwa ili kupunguza madhara kwa mazingira na binadamu.

 

Pia, napenda kutumia fursa hii kuukumbusha umma juu ya dhamira ya Serikali ya kupiga marufuku matumizi ya mifuko na vifungashio vya plastiki ifikapo Januari Mosi 2017.

 

Azma ya Serikali ya kupiga marufuku matumizi ya mifuko na vifungashio vya plastiki ni kuepusha athari za kiafya na mazingira zinazoendelea kujitokeza kutokana na matumizi ya mifuko hiyo. Hivyo basi wazalishaji, waagizaji, wasambazaji, wauzaji na watumiaji wa mifuko hiyo wanakumbushwa kuendelea na zoezi la kuondosha pamoja na kusitisha uzalishaji wa mifuko hii.

                                                IMETOLEWA NA

 JANUARY  Y. MAKAMBA (MB.)

WAZIRI WA NCHI OFISI YA MAKAMU WA RAIS

 MUUNGANO NA MAZINGIRA

 

 


 

<< Back to News Archive.