Kiswahili | English
Site Keyword Search:
    
 
Total site visits: 3960919.MAKAMU WA RAIS WA CUBA AHITIMISHA ZIARA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba Salvador Antonio Valdes Mesa ameondoka nchini mchana huu baada ya kumaliza ziara ya kiazi ya siku tatu kwa mwaliko wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan. 

Lengo la ziara hiyo ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba Salvador Antonio Valdes Mesa ni kuendeleza na kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Cuba hasa katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu,afya,utamaduni,michezo na utalii.

Katika sekta ya utalii, Serikali ya Cuba imeahidi  kuisaidia Tanzania katika kuendeleza utalii katika fukwe pamoja na kubadilishana uzoefu na wataalamu wa hapa nchini katika sekta hiyo ili kusaidia kuongeza pato la taifa kupitia shughuli  za utalii nchini.

Aidha kwenye sekta ya viwanda Tanzania na Cuba zimekubaliana kushirikiana katika ujenzi wa kiwanda cha kisasa cha kutengenezea madawa ya binadamu nchini.

Katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam,Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba Salvador Antonio Valdes Mesa ameagwa na mwenyeji wake Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan baada ya kuhitimisha ziara yake nchini.                   


 

<< Back to News Archive.