Kiswahili | English
Site Keyword Search:
    
 
Total site visits: 3957030.WAZIRI MAKAMBA ATEMBELEA MAABARA YA VYURA KIHANSI

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba amesisitiza umuhimu wa kutunza Vyanzo vya Maji kwakuwa shughuli zifanywazo na binadamu kando ya Vyanzo hivyo hupelekea mito hiyo kukauka.

hayo yamebainishwa leo na Waziri Makamba alipofanya ziara ya kikazi Kihansi Wilayani Kilolo kuangalia chanzo cha Mto Kihansi. Waziri Makamba kwa nyakati tofauti amefanya mazungumzo na wanakijiji wa Kijiji cha Mwantasi ambao wamefanya jitihada za dhati kuhifadhi Vyanzo vya Maji.

Waziri Makamba amewapongea na kuchangia kiasi cha shilingi laki mbili kwa vijiji vya Mwantasi kwa ajili ya Mfuko wa Mazingira wa Kijiji wenye lengo la kusimamia masuala za mazingira katika kijiji chao.

"Nawapongeza sana kwa jitihada mlizonazo ikiwa ni pamoja na kuwa na sheria ndogo ndogo za kutunza mazingira, nami nawaunga mkono kwa kuchangia kiasi cha shilingi laki moja kwa kijiji cha Mwantasi na laki moja kwa kijiji cha Wangama ili kuimarisha mfuko huo" Makamba alisisitiza.

Aidha Waziri Makamba amemuagiza Mkurugenzi wa Kilolo kuhakikisha fani zinazotozwa za uharibifu wa mazingira sehemu ya pesa hizo zinapelekwa katika vijiji husika ili kukuza mfuko huo na kuwaagiza wajumbe wa Kamati za Mazingira ngazi ya kijiji kuzitunza fedha hizo benki na kuagiza matumizi sahihi.

Waziri Makamba anaendelea na ziara ya kikazi katika Mikoa mbalimbali hapa nchini na leo yuko katika Mkoa wa Morogoro ambapo ametembelea Mto Kihansi na Ruaha Mkuu.


 

<< Back to News Archive.