Kiswahili | English
Site Keyword Search:
    
 
Total site visits: 3960968.WAZIRI MPINA ZIARANI KAHAMA

 MPINA AINYOOSHEA KIDOLE HALMASHAURI YA MJI KAHAMA

Maafisa watatu wasimamishwa kazi

SIKU moja baada ya Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muugano Mazingira Luhaga Mpina,kubaini ukiukwaji mkubwa wa usimamizi wa sheria za Mazingira na Baraza la Taifa la Mazingira (NEMC)kuiadhibu kulipa faini ya shilingi milioni 15,jana Naibu Waziri huyo amebaini umwagaji wa maji taka ovyo katika dampo la tala la Busoka mjini hapa.

Naibu waziri huyo katika ziara yake ya siku ya pili yenye staili ya
kushitukiza na kuachana na ratiba aliyopangiwa, alishuhudia uchafuzi wa mazigira wa gari moja aina la Fuso lenye namba za usajili T 245 BHC linalomilikiwa na Shule ya Msingi ya Kwema ya mjini Kahama lililokuwa likiendeshwa na Johanas Mwambeya,likimwaga maji taka kando ya barabara
karibu na dampo hilo.

Naibu Waziri huyo, aliyekuwa amefauatana na Wakaguzi wa Mratibu wa NEMC kanda ya Ziwa,Jamal Baruti, alisema kitendo hicho ni hujuma katika mazingira na ukiukwaji wa kifungu namba 187 cha utunzaji wa mazingira na kuagiza halmashauri hiyo ndani ya siku saba iwe imechimba bwawa maalum kwa ajili ya kumwaga maji taka na kutoa adhabu ya mmliki wa gari hilo kulipa shilingi milioni 1.2 ambazo mmiliki huyo alilipa mara moja.

“Ni jana tu adhabu ya shilingi milioni 15 imetolewa kwa halmashauri ya mji wa Kahama kwa ukiukwaji wa usimamizi wa sheria za utunzaji mazingira, na leo tunashuhudia uchafuzi mkubwa…..tumepita maeneo mengi hatujaona hali hii ya umwagaji vinyesi tena kando ya barabara na ni mchana kweupe….umwagaji katika eneo hilo la tambalare kuelekea katika vyanzo vya maji inasikitisha kweli kweli”Alisema Mpina.

“Hali hii inatafasiriwa kuwa halmashauri au serikali hii ndiyo
inayowapelekea wananchi wake magonjwa ya kuambukizwa kama kipindupindu na Typhoid…..huduma nzuri zinazo tolewa na serikali kwa wananchi wake sasa kwa mlango wa nyuma zinarudia wananchi kwa kuwaumiza….hili haliwezekani,hakika Mkurugenzi Kahama hili limeonyesha uzembe mkubwa
katika kusimamia usafi wa mazingira na huu sio watumishi wadogo ni wewe”Alisema Naibu Waziri huyo.

Naibu waziri huyo alisema kuwa hali hiyo imekuwa ikisababisha
uchafuzi mkubwa wa mazingira na hasa mkutitirisha maji machafu yenye kinyesi katika vyanzo vya maji vilivyo karibu na maeneo ya dampo hilo.

Alisema na kuagiza kuwa mara tu baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili wilayani Kahama angependa kusikia na kupata taarifa ndani ya siku saba kuwa tayari bwawa maalum linachimbwa kwa ajili ya kumwaga maji machafu.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri huyo, ameiagiza halmashauri hiyo kuacha mara moja kutupa taka katika uwanja wa wazi maarufu kama uwanja wa Magufuri uliopo eneo la Majengo mjini Kahama, na kuwa taka zote zilizopo ziondolewe na eneo la uwanja huo kuwa safi.

Kufuatia hali hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya mji wa Kahama Anderson Msumba,aliahidi kutekeleza agizo la Niabu Waziri huyo, huku akichukua hatua za kinidhamu za kuwasimamisha kazi baadhi ya maafisa katika ofisi yake kwa kile alichodai kuwa wakati hali hiyo ikitokea yeye alikuwa mapumzikoni katika likizo fupi.

Maafisa waliosimamisha kazi ni Mkuu wa Idara ya Usafishaji na
Mazingira,Martin Masele,Afisa Afya na Mazingira Johaness Mwabesi na Deogratias Dotto Afisa Afya.

Naibu Waziri mpina Pia alitembelea Mgodi wa kuzalisha Dhahabu wa Bulyankulu uliyopo Kahama na kujionea hali ya mazingira mgoni hapo Pamoja na kukagua mabwawa ya kisasa ya kuhifadhi maji taka yatokanayo na uzalishaji kiwandani hapo Mgodi umekuwa ukilalamikiwa na wakazi vya vijiji jirani kuwa wakati wa kipindi cha mvua mabwawa hayo hujaa maji na kwenda kwenye eneo la makazi ya watu na mazingira.

Naibu Waziri Mpina amelitaka Baraza la Taifa la Hifadhi na usimamizi wa Mazingira NEMC Kujiridhisha malalamiko hayo ya wananchi na kuagiza uongozi wa mgidi kuchukua hatua stahiki pamoja na kurekebisha mapungufu hayo iwapo yatabainika.


 

<< Back to News Archive.