Kiswahili | English
Site Keyword Search:
    
 
Total site visits: 4010370.WAZIRI MAKAMBA AKUTANA NA WATUMISHI WA IDARA YA MAZINGIRA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba hii leo amekutana na Wafanyakazi wa Idara ya Mazingira katika Ofisi yake na kuwataka kufanya kazi kwa weledi na kuandika maandiko mbalimbali ili kupata fedha za kuratibu miradi ya mazingira nchini.

Waziri Makamba amewataka watumishi hao kuacha kufanya kazi kwa mazoea bali kujenga dhana ya uwajibikaji kwa kila mmoja ili kuacha alama kwa yale mazuri yanayofanywa ili iwe kumbukumbu kwa vizazi vya sasa na vizazi vijavyo.


 

<< Back to News Archive.