Mhe Samia afungua Mkutano Mkuu wa Elimu Maalumu Lushoto mkoani Tanga

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo Julai 15, 2019 amefungua Mkutano Mkuu wa 16 wa Nusu Mwaka wa Taasisi ya Kimataifa ya Elimu Maalumu (International Association of Special Education (IASE) wilayani Lushoto mkoani Tanga.

Mkutano huo umefanyika leo katika Chuo Kikuu cha kumbukumbu ya Sebastian Kolowa (SEKOMU) katika kijiji cha Magamba Wilayani humo.

Mhe. Samia pia alitumia nafasi hito kusalimiana na kuzungumza na Washiriki wa Mkutano huo.

Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.