MAKATIBU WAKUU WA TANZANIA BARA NA ZANZIBAR WAKUTANA KUJADILI MASUALA YA MUUNGANO

[:en]Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Joseph Malongo (kushoto) akiendesha kikao kazi cha Makatibu Wakuu kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ). Pamoja na mambo mengine kikao hicho kimejadili juu ya uratibu na ufuatiliaji wa masuala ya Muungano. Kulia ni Bw. Abdallah Mitawi Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais ambae ni Mwenyekiti Mwenza. Kikao hicho kimefanyika hii leo katika Ukumbi wa Hazina, Jijini Dodoma.[:]