Naibu Waziri Kangi Lugola azindua warsha ya mradi wa kuhimili mabadiliko ya Tabianchi

[:en]Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Kangi Lugola akifungua warsha ya uzinduzi wa Mradi Mkubwa kusaidia kuhimili mabadiliko ya tabianchi katika Wilaya nne za Tanzania Bara ambazo ni Mvomero, Kishapu, Mpwapwa na Simanjiro. Mradi huo pia utatekelezwa katika Wilaya moja Tanzania Visiwani ambayo ni Kaskazini Unguja A-Shehia. Mradi huo mkubwa una thamani ya kiasi cha Dola za Marekani 7,571,233 unategemea kutekelezwa ndani miaka mitano.[:]