Ofisi ya Makamu wa Rais yazindua Mpango Kazi wa Taifa wa Afya na Mazingira

Ofisi ya Makamu wa Rais Julai 19, 2019 imezindua Mpango Kazi wa Taifa wa Afya na Mazingira (HPAP) jijini Dodoma wenye lengo la kutatua changamoto za afya kutokana na uharibifu wa mazingira.

HPAP ambayo imeandaliwa kwa kushirikishiana na Wizara ya Afya, Maendeleo yya Jamiii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na wadau umeainisha viashiria vitano vya uchafuzi wa mazingira vinaathiri afya hivyo imepatikana njia ya kubuni miradi ya kupambana nazo.

Akizungumza baada ya uzinduzi, Mkurugenzi Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Profesa William Mwegoha alisema ripoti ya Shirika la Afya Duniani (WHO) ya mwaka 2015 inaonesha wastani wa vifo milioni 8 duniani hutokana uchafuzi wa mazingira.

Alisema pia takriban asilimia 19 ya vifo duniani vinatokana na changamoto hizo za kimazingira na hivyo Mpango huo utaleta mwelekeo wa kuzitatua changamoto hizo.

Prof. Mwegoha ambaye alimwakilisha Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Balozi Joseph Sokoine alisema afya ya nguvu kazi ni muhimu na ili tuweze kuwa na uchumi thabiti ni lazima afya ipatikane.

“Kama nchi tulisaini Mkataba wa Libreville mwaka 2008 ambao tukatakiwa kama nchi tutengeneze mpango kazi wa namna ya kupambana na changamoto za kiafya kutokana na uchafuzi wa mazingira hivyo unatupa nafasi ya kuja na miradi na kutusaidia sisi Watanzania kupambana nazo,” alisema.

Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi Idara ya Mazingira wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Viwanda (UNIDO), Nilgue Tas alisema huu ni wakati wa wadau nchini na washirika wa maendeleo kueleza uzoefu wao kuhusu madhara ya uchafuzi wa mazingira.

Tas alisema HPAP inatokana na ushiriki wa wadau ambapo Serikali ya Tanzania ikiandaa miradi kwa ajili ya kutatua changamoto hizi za uchafuzi wa mazingira hatari kwa afya.

Mwakilishi Mkazi wa UNIDO, Dkt. Stephen Kargbo alisema Shirika hilo litaendelea kufanya kazi na wadau wote ili kufanikisha maendeleo nchini kupitia taasisi mbalimbali za Serikali.

“Ninatambua juhudi za Tanzania katika kutatua changamotto za afya na mazingira kwa mfano mwaka 2013 Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais na Wizara ya Afya pamoja na wadau ikishirikiana na WHO iliandaa Mpango Kazi uliolenga kutatua changamoto hizi,” alisema Kargbo.

HPAP imewezeshwa na UNIDO ikishirikiana na wadau wa Usafi Tanzania (CPCT) na WHO chini ya ufadhili wa Umoja wa Ulaya (EU) na Shirika la Maendeleo la Mare


kani (USAID).