TAARIFA KWA UMMA

 

 

TAARIFA KWA UMMA

UTARATIBU WA KUOMBA KIBALI CHA KUKUSANYA NA KUSAFIRISHA TAKA HATARISHI NCHINI TANZANIA

Ofisi ya Makamu wa Rais imeboresha utaratibu wa maombi ya vibali vya ukusanyaji, usafirishaji, urejelezaji na uteketezaji, wa taka zenye madhara kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Miongozo. Taka hizo ni pamoja na vyuma chakavu, mafuta machafu (Oil chafu), matairi yaliyotumika, taka za kieletroniki na taka zitokanazo na kemikali.

Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya Mwaka 2004 pamoja na kanuni za usimamizi wa taka hatarishi za Mwaka 2009 Kifungu 15, 42 na 43 inatoa utaratibu unaotakiwa kuzingatiwa katika kukusanya, kusafirisha, kuhifadhi, kuteketeza na kurejereza taka kwa lengo la kuepusha madhara ya kiafya na kimazingira yanayoweza kusababishwa na taka hizo.

Kwa minajili hiyo, mtu binafsi, kampuni au kiwanda anatakiwa kuandika barua ya maombi ya kibali hicho kwa Mkurugenzi wa Mazingira yakiambatana na nyaraka zifuatazo:-

  1. Fomu za maombi
  2. Ripoti ya ukaguzi
  • Leseni ya biashara
  1. TIN namba
  2. Maelezo ya kampuni husika
  3. Mkataba unaoonyesha sehemu anayochukulia taka na anakopeleka kwa madhumuni ya kurejereza au kuteketeza.
  • Kwa wale wenye mitambo ya kuteketezea/kurejereza taka, waambatishe cheti cha tathimini kwa athari za mazingira.
  • Kwa wanaoomba “renewal” watatakiwa kuwasilisha “Return Forms” zinazoeleza ni kiasi gani cha taka zilikusanywa kupitia leseni iliyokwisha muda wake.

Fomu za maombi zinapatikana Ofisi za NEMC zilizoko kwenye kanda, makao makuu, Halmashauri zote au tovuti ya Ofisi ya Makamu wa Rais www.vpo.go.tz

 

 

Mhandisi Joseph K. Malongo

KATIBU MKUU

25 Juni, 2018