Kiswahili | English
Site Keyword Search:
    
 
Total site visits: 3712292.
Click on the thumb to view the photo

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Mohammed Gharib Bilal, akijaribu kuvaa miwani ili kuweza kuona picha iliyokuwa ikionyeshwa ukutani kupitia Screen na Projector (Animation Fils) , wakati alipotembelea Banda la maonyesho baada ya kufungua mkutano wa sita wa Kimataifa wa Afrika kuhusu Teknolojia ya Taarifa na Mawasiliano ya Ustawi, Elimu na Mafunzo (ICT), uliofunguliwa kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam jana Mei 25. Kushoto ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka na Waziri wa Elimu na Mafunzo, Shukuru Kawambwa (kulia) ni Mkurugenzi wa Designmate Animation Films, Colonel Basavaraj.
Picha ya pamoja na baadhi ya watu waliopresent paper zao.
Baadhi ya Mawaziri na Manaibu wao waliohudhuria ufunguzi wa mkutano huo, wakifuatilia maonyesho ya picha zilizokuwa zikionyeshwa katika Screen za ukutani. 08:- Waziri wa Elimu wa na Mafunzo ya Ufundi, Shukuru Kawambwa, akizungumza baada ya makamu wa rais kufungua mkutano huo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihojiwa na waandishi wa habari baada ya kufungua mkutano huo wa sita wa Kimataifa wa Afrika kuhusu Teknolojia ya Taarifa na Mawasiliano ya Ustawi, Elimu na Mafunzo (ICT), uliofunguliwa jijini Dar es Salaam Mei 25.

«Back to the list of Albums