Kiswahili | English
Site Keyword Search:
    
Total site visits: 3711981.
Click on the thumb to view the photo

Sehemu ya watanzania waishio New York na vitongoji vyake, wakianza kukusanyika kwa ajili ya kujiandaa kumpokea Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, kwa ajili ya kukutana na kuzungumza nao Juni 11, 2011.
Katika hafla hiyo hata viongozi wa Jumuiya hiyo hawakuwa nyuma katika kutekeleza majukumu yao kama kawaida japo ilikuwa ni jumapili, hapa ni Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Miriam Abu (kushoto) na Mweka hazina msaidizi, Mzee Temba, wakiwa na nyaraka zao ambapo pia walikuwa wakiendelea na zoezi la kusajiri Watanzania wapya waliokuwa wakitaka kujiunga na Jumuiya hiyo.
Jumuiya hiyo ilianza kuwa active zaidi baada ya uchaguzi mkuu wa kuchagua viongozi wa kuiongoza uliofanyika mwezi April mwaka huu na kuwapata viongozi wapya kama Mwenyekiti, Haji Hamis na Makamu wake huyo, Katibu Vicent Mughwai na Katibu msaidizi, Shaban Mseba na Mweka Hazina, Phillip Lwiza na msaidizi wake, Mzee temba na sasa Jumuiya hiyo imejipangia majukumu na malengo mengi ikiambatana na mikakati kabambe ya kuwawezesha kusonga mbele katika kujikwamua kiuchumi na kuweza kusaidiana kimaisha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal na mkewe, Mama Zakhia Bilal, Balozi Obeni Sefue na Waziri Juma Duni Haji, wakisimama na kuimba wimbo wa maalum baada ya kuwasili kwenye eneo la hafla hiyo.
Baadhi ya Watanzania waishio New York na vitongoji vyake wakimsikiliza kwa makini Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed gharib Bilal, alipokuwa akiwahutubia.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania waishio New York na vitongoji vyake, Haji Hamis, akizungumza na kutoa utambulisho wa viongozi na wanachama wa Jumuiya hiyo, ambao hadi sasa wamefiki 110.

«Back to the list of Albums