WILAYA TANO KUNUFAIKA NA MRADI MKUBWA WA KUHIMILI MABADILIKO YA TABIANCHI

Katika jitihada za kuhimili Mabadiliko ya tabianchi Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais imepata fedha kutoka Mfuko wa Mazingira Duniani (Global Environmental Facility – GEF) kiasi cha Shilingi Bilioni 16 kwa ajili ya kutekeleza mradi wa Kusaidia Kuhimili Mabadiliko ya tabianchi (Ecosystem Based Adaptation for Rural Resilience (EBARR) in Tanzania).

Aidha, akizundua mradi huo, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Kangi Lugola amesema kuwa ni faraja kubwa kwa Ofisi yake yenye jukumu la kuratibu masuala ya Usimamizi wa Mazingira Nchini kupata mradi huo wenye manufaa kwa taifa.

Waziri Lugola amebainisha kuwa, lengo la mradi huo ni kujenga uwezo wa kuhimili Mabadiliko ya tabianchi kwa maeneo ya vijijini ambayo kwa kiasi kikubwa bado hayajifikiwa na miradi mikubwa. Vilevile, kubaini athari za mabadiliko ya tabianchi, kuwezesha wananchi kulima mazao yanayohilimi ukame na ufugaji endelevu wenye lengo la kuboresha kipato.

Aidha, Naibu Waziri Lugola amesema kuwa katika kutekeleza mradi huu kiasi cha Shilingi Bilioni 6 zimeelekezwa katika Wizara ya Kilimo, ili kuratibu usimamizi endelevu wa kilimo katika program maalumu inayoitwa Kilimo kinachohimili Mabadiliko ya tabianchi (Climate Smart Agriculture). Mradi huo pia unalenga kuwapatia maji safi na salama wakazi wa maeneo mradi utakapo tekelezwa kupitia uchimbaji wa visima, ujenzi wa mabwawa, uvunaji wa maji ya mvua na Kilimo cha umwagiliaji kwa vikundi endelevu. “Naagiza Vikundi vijengewe uwezo, visajiliwe na vitambulike, Waziri Lugola alisisitiza.”

Ofisi ya Makamu wa Rais ndio Mratibu Mkuu wa mradi huu ambao unatekelezwa katika Wilaya Nne za Tanzania Bara na Wilaya moja ya Tanzania Visiwani. Wilaya zitakazo nufaika na mradi huu ni pamoja na Kishapu iliyopo Mkoani Shinyanga, Mpwapwa- Dodoma, Simanjiro-Manyara na Mvomero iliyopo Mkoani Morogoro na Kaskazini Unguja – Shehia A